Matthew 14:8-11

8Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” 9Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. 10 aHivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani. 11Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake.
Copyright information for SwhNEN